Karibu Shimmuta

Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania

Habari Picha

  • Kamati ya Utendaji ya SHIMMUTA inawasilisha ombi kwa Mashirika, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania kurejea kushiriki katika michezo hii ambayo itatoa fursa kwa wafanyakazi kukutana na kushiriki michezo na wafanyakazi wengine kutoka nchi nzima ili kuamsha ari ya ushirikiano kama malengo ya sera ya Maendeleo ya Michezo ya Taifa yalivyo. Shimmuta Admin
  • Uongozi wa Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) katika Mkutano wake wa Halmashauri Kuu uliofanyika tarehe 08 Aprili, 2022, katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma (IRDP) uliazimia kuwa, michezo ya Shirikisho kwa mwaka 2022 itafanyika Mkoani Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani kuanzia tarehe 15 hadi 29 Novemba, 2022. Shimmuta Admin
  • Michezo itakayoshindaniwa itakuwa Mpira wa Miguu, Netiboli, Kuvutana Kamba, Kukimbia Mtu akiwa Ndani ya Gunia, Riadha, Vishale (Darts), Mpira wa Wavu, Mpira wa Kikapu, Pool Table, Drafti, Bao na Karata. Mgeni Rasmi kwenye ufunguzi wa Michezo ya Mwaka huu Mkoani Morogoro, atakuwa Mlezi wetu, Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Shimmuta Admin
  • MUHIMU: Mashindano haya yanahusisha Wafanyakazi tu. Hivyo, wanamichezo ambao sio Wafanyakazi wa Taasisi/Shirika/Kampuni yako maarufu kama “Mamluki” hawaruhusiwi kabisa kushiriki kwenye michezo hii. Hivyo, inahimizwa kila Mfanyakazi aje na Kitambulisho chake cha kazi halisia zikiwemo “Salary Pay Slips” za miezi miwili kabla ya mashindano. Shimmuta Admin
  • MKUTANO MKUU WA 56 WA HALMASHAURI KUU YA SHIMMUTA WAFANYIKA JIJINI ARUSHA. Makamu mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof Epaphra Manamba leo tarehe 4/4/2024 amefungua mkutano mkuu wa 56 wa halmashauri kuu ya SHIMMUTA unaofanyika katika Chuo hicho (IAA). Prof Manamba amepongeza jitihada mbalimbali zinazofanywa na SHIMMUTA katika kuhakikisha watumishi wanashiriki katika shughuli za michezo kazini. Naye Mwenyekiti wa SHIMMUTA Bi Roselyne Massam amesema Mkutano Mkuu wa 56 wa Halmashauri kuu umejikita katika kujadili mpango mkakati wa shirikisho, Sera ya michezo kazini na kujadili taarifa ya mashindano ya SHIMMUTA yaliyofanyika mwaka 2023 jijini Dodoma. Mkutano huo unafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 4 – 5 Aprili 2024 katika ukumbi wa utawala katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Shimmuta Admin

Washirika wetu