Maombi kwa Mashirika, Taasisi na Makampuni Kujiunga
Kamati ya Utendaji ya SHIMMUTA inawasilisha ombi kwa Mashirika, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania kurejea kushiriki katika michezo hii ambayo itatoa fursa kwa wafanyakazi kukutana na kushiriki michezo na wafanyakazi wengine kutoka nchi nzima ili kuamsha ari ya ushirikiano kama malengo ya sera ya Maendeleo ya Michezo ya Taifa yalivyo. Ushiriki wa wafanyakazi kwenye michezo utachochea uchapa kazi sehemu za kazi na kuimarisha afya za wafanyakazi, bidii na nidhamu ya wafanyakazi hao sehemu za kazi.
Kujiunga kwa Shirika/Taasisi/Kampuni yako na kushiriki kwenye mashindano ya mwaka huu, kutakuwa na faida zifuatazo:-
- Michezo huimarisha afya za wafanyakazi mahala pa kazi;
- Michezo huwezesha Wafanyakazi waweze kuzalisha kwa tija zaidi na kutoa huduma bora iliyotukuka;
- Michezo husaidia kuwakutanisha wafanyakazi, kufahamiana na kubadilishana uzoefu;
- Michezo hutangaza jina/biashara/huduma nzuri inayozalishwa au kutolewa na Shirika/Taasisi/Kampuni;
- Michezo sehemu za kazi, hukuza vipaji na kuwezesha kupata wanamichezo wanaoweza kuchezea timu mbali mbali za Taifa;
- Kutimiza haki na wajibu wa mfanyakazi kupitia michezo.