MICHEZO YA SHIMMUTA KWA MWAKA 2022

Uongozi wa Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) katika Mkutano wake wa Halmashauri Kuu uliofanyika tarehe 08 Aprili, 2022, katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma (IRDP) uliazimia kuwa, michezo ya Shirikisho kwa mwaka 2022 itafanyika Mkoani Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani kuanzia tarehe 15 hadi 29 Novemba, 2022.

Michezo itakayoshindaniwa itakuwa Mpira wa Miguu, Netiboli, Kuvutana Kamba, Kukimbia Mtu akiwa Ndani ya Gunia, Riadha, Vishale (Darts), Mpira wa Wavu, Mpira wa Kikapu, Pool Table, Drafti, Bao na Karata. Mgeni Rasmi kwenye ufunguzi wa Michezo ya Mwaka huu Mkoani Morogoro, atakuwa Mlezi wetu, Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.