Karibu Shimmuta
Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania.
Maono
Shirikisho hili limesajiliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 12 cha Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa ya Mwaka 1967, ili kuanzisha mashindsno mbalimbali.
Dhima
Kuendesha na kusimamia Mashindano ya Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi hapa nchini.
Matarajio
Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Taifa ya Mwaka 1995 inasisitiza kushiriki katika michezo ili kujenga mshikamano wa kitaifa kupitia michezo mbalimbali.
Mafanikio
Kupitia michezo mbalimbali inaypfanyika kila mwaka, Shimmuta imefanikiwa kuwaleta watu pamoja na kuongeza mshikamano na mahusiano mazuri.
Historia
SHIMMUTA ni miongoni mwa Mashirikisho manne ya Michezo yaliyoanzishwa na Serikali ya Awamu ya Kwanza iliyoongozwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere mnamo Mwaka 1967. Mashirikisho mengine yaliyoanzishwa ni pamoja na SHIMIWI (Shirikisho la Michezo ya Idara na Wizara za Serikali), SHIMISEMITA (Shirikisho la Michezo ya Serikali za Mitaa) na BAMATA (Shirikisho la Michezo ya Majeshi Tanzania).
Mashirikisho haya ya Michezo yote kwa pamoja yameshirikishwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na hufanya Mashindano yake kila Mwaka kuligana na ratiba inayopangwa na Mashirikisho yenyewe na kuidhinishwa na Baraza la Michezo ya Taifa (BMT). Kwa upande wa SHIMMUTA ratiba ya Mashindano iliyotolewa na BMT ni michezo kufanyika kila Mwezi Novemba ya kila Mwaka.
UENDESHAJI WA SHIMMUTA
Shirikisho hili limesajiliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 12 cha Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa ya Mwaka 1967 yaani “The National Sports Council of Tanzania Act No. 12 of 1967”. Dhima ya uanzishwaji wa SHIMMUTA ilikuwa ni kuendesha na kusimamia Mashindano ya Mashirika ya Umma pekee wakati ule. Lakini kutokana na Sera ya ubinafsishaji iliyotekelezwa na miaka ya tisini na kupelekea kubinafsishwa kwa baadhi ya Mashirika ya Umma Baraza la Michezo la Taifa lilielekeza SHIMMUTA kushirikisha pia Taasisi na Makampuni Binafsi hapa nchini.
Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Taifa ya Mwaka 1995 inasisitiza katika Taifa linaloshiriki katika Michezo ili kujenga uhusiano, uelewano na mshikamano wa kitaifa kupitia michezo mbalimbali. Sera imeelekeza katika kifungu cha 5 kuwa vyombo vyenye jukumu la kutekeleza Sera ya Michezo ni pamoja na Mashirikisho ya michezo (ikiwa ni pamoja na SHIMMUTA). Hivyo, kwa maudhui ya Sheria, michezo kwa wafanyakazi mahali pa kazi siyo hiari bali ni takwa la kisheria.
Timu ya Wasimamizi

Bi Roselyne Massam
Mwenyekiti
Maswet Masinda
Katibu Mkuu
Issa Hamisi Issa
Naibu Katibu Mkuu