Shimmuta inajumuisha michezo ya aina mbalimbali
Kwa mwaka huu 2021 michezo itakayoshindaniwa itakuwa Mpira wa Miguu, Netiboli, Kuvutana Kamba, Kukimbia Mtu akiwa Ndani ya Gunia, Riadha, Vishale (Darts), Mpira wa Wavu, Mpira wa Kikapu, Pool Table, Drafti, Bao na Karata. Mgeni Rasmi kwenye ufunguzi wa Michezo ya Mwaka huu Mkoani Morogoro, atakuwa Mlezi wetu, Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.